Waziri wa Elimu, Sanyansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, ameagiza walimu wote walioanzisha vituo vya mafunzo ya ziada (tuition) wakati ambao shule zote zimefungwa kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona watiwe mbaroni.

Ametoa agizo hilo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma na kuwataka wanafunzi waliopo nyumbani kuacha kuzurura ili kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo Kwani kwa sasa Serikali inahamasisha wanafunzi kuepuka mikusanyiko mfano Twisheni, vikundi vya majadiliano, vibanda vya video, na mashindano ya michezo na kuhimiza wanafunzi hao kubaki nyumbani na kuendelea kujisomea.

Hivyo amewaagiza wakurugenzi, wakuu wa wilaya na mikoa kuwachukulia hatua wale wote walioanzisha vituo vya mafunzo ya ziada.

“Wanafunzi watambue kuwa hiyo si likizo bali wamerudi nyumbani kwasababu ya janga kubwa linaloitesa dunia la virusi vya corona. Kuna baadhi ya sehemu baada ya kusikia watoto wapo nyumbani wameanzisha ‘tuition’. Nawataka wote walioanzisha ‘tuition’ waache mara moja,” alionya.

Aidha amewataka walimu wakuu kutowaruhusu wanafunzi kukusanyika katika maeneo ya shule kwa kipindi chote ambacho shule zimefungwa.

Tahadhari nyingine iliyotolewa, inaitaka jamii iwalinde wanafunzi na watoto wote katika maeneo yao kwa kuhakikisha hawaendi katika maeneo hatarishi yakiwamo yenye msongamano.

Kadhalika wametahadharisha wazazi na walezi wazungumze na watoto wao kuhusu njia za kujikinga na virusi vya corona na kuwasaidia kuendelea kujisomea wakiwa nyumbani.

Rwanda: Wanajeshi watuhumiwa kubaka raia, Amri ya Karantini
Serengeti: Mwanafunzi afariki kwa kukanyagwa na Tembo