Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Angellah Kairuki ametaka kila mwalimu nchini aendelee kuthaminiwa na kulindiwa utu wake.

Kairuki ametoa wito huo hii leo Machi 16, 2023 wakati wa ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Utumishi wa Walimu – TSC, katika Ukumbi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dodoma.

Amesema, “ni wajibu wenu kuhakikisha maslahi ya walimu na hadhi yake inalindwa kwa nguvu zote, pia tutambue mchango wao, ili waweze kuleta mabadiliko ya elimu bora nchini kwa kuwahamasisha kutimiza wajibu wao, kulinda masilahi yao, kuwaondolea kero na malalamiko yao,” amesema Kairuki.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Angellah Kairuki.

Aidha, Kairuki ameongeza kuwa amezisikia changamoto zinazoikabili Tume ya Utumishi wa Walimu ambazo zimeelezwa na Mwenyekiti wa Baraza, hususani ukosefu wa jengo la ofisi ya Makao Makuu.

“Nimeona jitihada mlizozifanya na hatua za ujenzi zilishaanza. pia, nimepata taarifa kuwa mradi wa jengo la tume umeingizwa katika utaratibu wa miradi inayosimamiwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, kasi ya ujenzi imefikia asilimia tano badala ya asilimia 16 kama inavyoonesha na ujenzi unatarajia kukamilika Juni 5, 2024,” amesema Kairuki.

Hata hivyo, amesema kuwa, “Naielekeza Kandarasi ya SUMA JKT ihakikishe kuwa ujenzi wa Jengo la Tume ya Utumishi wa Walimu unakamilika kwa wakati, kwa kuwa jengo wanalotumia kwa sasa haliendani na majukumu wanayoyafanya katika kuwahudumia Walimu nchini.

Chalamila amuomba Rais kufungua vyuo vilivyofungiwa
Rais Samia amteuwa Kusaya kuwa Katibu Tawala