Mwanafunzi wa kidato cha pili Sekondari ya Kayanga iliyopo wilaya ya Karagwe mkoani Kagera, amefanyiwa ukatili na walimu wake wawili baada ya kumpiga na kuchoma moto viganja vya mikono na miguuni kwa madai ya kutoroka bwenini.

Mkuu wa shule hiyo, Johnbosco Paul amekiri kutendeka kwa tukio hilo shuleni kwake na kwamba asingependa kulizungumzia kwa kuwa tayari limefikishwa polisi.

Ofisa ustawi wa jamii Wilaya ya Karagwe, Owokusiima Kaihura amesema alipata taarifa za mwanafunzi huyo kuwa amelazwa zahanati binafsi ya Family kutokana na kuunguzwa moto na walimu wake.

“Nilipofika kwenye zahanati hiyo nilimpeleka katika Kituo cha Afya Kayanga kisha nikatoa taarifa polisi kuhusu tukio hilo. Nitaendelea kufuatilia mwenendo wa kesi hiyo,” amesema Kaihura.

Mama mzazi wa mtoto huyo, Mchungaji Upendo Simba amesema kuwa amesikitishwa sana na kitendo cha mwanae kuunguzwa hivyo analiachia jeshi la polisi lifanye kazi yake.

Kwa upande wake mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kayanga, Mika Makanja ili kuzungumzia suala hilo licha ya kukiri kuwapo kwa tukio hilo, amesema hawezi kulitolea ufafanuzi kwa sababu yupo nje ya kituo cha kazi.

Hata hivyo, Waraka wa Wizara ya Elimu kuhusu utoaji adhabu kwa wanafunzi, unataka warekebishwe tabia ili wawe viongozi wazuri.

Mwakyembe azindua Baraza la Michezo la Taifa la Kumi na nne
Nicki Minaj afichua siri, aitangaza tarehe yake