Sakata la Watumishi hewa katika kada mbalimbali limeendelea kuwagharimu watendaji Serikalini tangu Rais John Magufuli alipotangaza vita dhidi yao.

Uchunguzi uliofanywa katika Halmashauri ya Wilaya ya Hai, umewabaini na kupelekea kuwajibishwa vikali kwa watumishi watatu wa Halmashauri hiyo waliotumia mishahara ya watumishi hewa kujizolea mikopo ya jumla ya shilingi milioni 35.2 katika Benki ya CRDB.

Akizungumza katika kikao cha Baraza hilo jana, Mwenyekiti wa Halashauri hiyo, Helga Mchomvu alisema kuwa Baraza hilo limeamua kuwafukuza kazi watumishi hao.

Mchomvu aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Mkuu Idara ya Utumishi na Utawala, Gudila Mashele, Ofisa Utumishi Daraja la Kwanza, Faraja Ndatu na Mchumi Daraja la Pili, Isaiah Bayege.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti huyo alieleza kuwa Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo limewafukuza kazi watumishi wengine waliobainika kuiba fedha za muda wa ziada (Extended Duty Allowance) za madaktai wa Hospitali ya Machame, zaidi ya shilingi milioni 24.

Aidha, Wahasibu pamoja na dereva wa Halmashauri hiyo wamefukuzwa kazi baada ya kubainika kuwa walishiriki katika malipo hewa ya dawa za hopitali hiyo zenye gharama ya zaidi ya shilingi milioni 32.

Rungu hilo pia limewashukia watumishi wengine ambao wamejikuta wakishushwa vyeo baada ya kubainika kuwa walifanya makosa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kugushi nyaraka za kuidhinisha malipo.

Video Mpya: Lady Jay Dee - Ndindindi
Nape awafungukia wapinzani baada ya kususia Bunge