Leo Agosti 14, 2018 Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imefanya mkutano na kuteua wagombea wa CCM katika uchaguzi mdogo wa Ubunge kilichofanyika katika ofisi ndogo ya makao makuu Lumumba Jijini Dar es salaam kikiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli.

Ambapo katika mkutano huo kamati imewateua wabunge waliojiuzulu Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kuunga mkono jitihada za Rais John Pombe Magufuli (CCM) kamati imewateua wagombea hao kugombea tena majimbo yao wakiwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi.

Julius Kalanga Laizer aliyekuwa mbunge wa jimbo la Monduli ameteuliwa tena kugombea ubunge jimboni hapo lakini pia kamati imemteua Mwita Mikwabe Waitara kugombea ubunge jimbo alilokuwa mbunge kwa tiketi ya Chadema Ukonga.

Aidha Timotheo Paul Mzava ameteuliwa kugombea jimbo la Korogwe vijijini lililokuwa linashikilkiwa na Stephen Ngonyani Majimarefu aliyefariki dunia akipatiwa matibabu katika hospitali ya Muhimbili.

 

DC Ilala atoa agizo la kupeleka TAKUKURU kuchunguza mradi wa upimaji Kipunguni
Marekani, Paraguay, Costa Rica, Mexico zapigana vikumbo kwa Sampaoli

Comments

comments