Jeshi la Polisi nchini India linawashikilia watu watano wanaoaminika kuhusika moja kwa moja kumdhalilisha msichana wa Kitanzania aliyoko masomoni nchini humo kwa kumvua nguo barabarani na kuchoma moto gari walilokuwa wakisafiria katika jimbo  la Bangalore.

Balozi wa Tanzania nchini humo, Mhandisi, John Kijazi ameeleza kuwa Serikali ya Tanzania iliiandikia dokezo serikali ya India kuitaka kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watu waliohusika na tukio hilo, na kwamba tayari wamepewa taarifa kuwa wamewatia mbaroni waliohusika.

Balozi Kizaki ameeleza kuwa baada ya kuiomba serikali ya India kutoa taarifa za kina kuhusu tukio hilo, imebainika kuwa wa watanzania wanne ambao ni wanafunzi ndio walioathirika na tukio hilo ambapo watatu kati yao ni wanaume.

“Serikali ya India imeanza kuchukua hatua. Kwanza imeimarisha ulinzi pale kwenye eneo walapoishi wanafunzi kwa sababu wale wenyeji bado wanatishia kuwadhuru wanafunzi wale, kwa sababu bado walikuwa na hasira za kuuawa kwa yule mama ambaye aligongwa na gari ambayo ilikuwa inaendeshwa na dereva mwanafunzi wa Sudan… wala sio Mtanzania,” alisema Balozi Kizaki.

“Taarifa ambazo tumezipata ni kwamba wameshakamatwa watu watano kuhusiana na tukio hilo, na uchunguzi uchunguzi unaendelea,” aliongeza.

Balozi huyo alieleza kuwa wameitaka Serikali ya India kuwaelimisha wananchi wao kwani baadhi yao bado wana tabia za kibaguzi kwa wageni hasa wanaotoka Afrika. Alisema vitendo vya unyanyasaji kwa wanafunzi wa Afrika vimekuwa vikitokea mara kwa mara vikifanywa na wenyeji.

Serikali ya Tanzania imelaani vikali kitendo hicho cha kidhalilishaji.

Misana Mayingu, mwanafunzi Mtanzania anaesoma nchini India ameeleza kuwa hivi sasa hofu ya kushambuliwa na wenyeji imeongezeka licha ya kuwepo na ulinzi kutoka kwa jeshi la polisi la India katika maeneo yao na kupewa ruhusa ya kutoka nje.

Magufuli aahidi kuendeleza 'minyoosho', asema yeye sio kichaa, Dikteta
Lowassa atoa ombi lake kwa Rais Magufuli, Bado anauona mlango wa ikulu