Mahakama Kuu kanda ya Mwanza imewahukumu kunyongwa hadi kufa, washtakiwa wanne kati ya saba baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza (RPC) Liberatus Barlow October, 2012.

Hukumu hiyo imetolewa Mwanza na Jaji Sirialus Matupa baada ya Mahakama kuridhika bila shaka yoyote na ushahidi uliowasilishwa kuwa Watuhumiwa hao wanne kati ya saba walitenda kosa hilo.

Waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa ni Muganyizi Michael, Magige Mwita, Abdallah Petro na Abdulrhaman Ismail.

Walioachiwa huru na Mahakama baada ya ushahidi kutowatia hatiani katika kesi hiyo ya mauaji namba 192/2014 ni Chacha Mwita, Buganizi Edward na Bhoke Marwa.

Kamanda Barlow aliuawa kwa kupigwa risasi katika tukio lililotokea eneo la Kitangiri Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza saa 8:00 usiku wa kuamkia Oktoba 13, 2012.

Moto ulioanzia chumba cha watoto wateketeza Hospitali ya Mombasa
Seneta wa upinzani ajitangaza kuwa Rais Bolivia

Comments

comments