Magunia 30 ya karafuu yaliyokuwa yamefichwa kisiwa cha Funzi Wilayani Wete, Kaskazini Pemba yamekamatwa na Kikosi Maalumu Cha Kuzuia Magendo (KMKM).

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omar Khamis Othman, ameagiza karafuu zilizokamatwa ziuzwe ili wahusika waliotoa taarifa wapatiwe mgao kama motisha ya kuweza kuendelea kufichua vitendo vya kimagendo.

Karafuu hiyo inasadikiwa kuwa ilikuwa katika hatua za kusafirishwa kwenda kuuzwa nje ya nchi kimagendo.

RC Othman amesema Serikali inaridhishwa na utendaji kazi wa kikosi hicho na kuwataka kuendelea kudhibiti biashara ya magendo ili wahusika wapatikane na kuchukuliwa hatua.

Kesi za mauzo ya silaha na Rushwa zaendelea kumtesa Zuma kizimbani
Mastaa FC Barcelona watibuana, kocha aingilia kati