Mkuu wa Mkoa wa Songwe,  Chiku Galawa ameagiza viongozi wa serikali za vijiji na kata kuwakamata vijana wote wanaokimbilia mijini na kuacha  kuwahudumia wazazi wao ili washughulikiwe kwa kosa la kuwatelekeza.

Ameyasema hayo leo katika Kijiji cha Zelezeta Wilayani Mbozi mkoani humo alipotembelea wanufaika wa mradi wa mpango wa kunusuru kaya masikini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf).

Amesema kuwa lazima serikali za vijiji na kata zichukue hatua kwa vijana wa aina hiyo kwani wanafahamika ili kuwalazimisha kutimiza wajibu wao wa msingi wa kulea familia zao lakini pia kulea wazee wao ambao walitumia nguvu nyingi kuwalea  wao wakiwa vijana.

“Hakuna mwenye hati miliki ya ujana kila mmoja ni mzee mtarajiwa, kama ukishindwa kulea wazazi wako leo wanao wanakuona nawe hawatakulea utakapokuwa mzee hivyo kuweni na upendo waleeni wazee, pia vijana acheni tabia ya kuzaa bila mpango na kuwatelekeza watoto wenu tumieni rasilimali ardhi mliyonayo kujipatia kipato,” amesema Galawa

Aidha, Galawa ametoa mwezi mmoja kuanzia leo Alhamisi kwa halmashauri zote mkoani humo kuwalipia bima ya afya (CHF) wazee wote ili waweze kutibiwa wanapohitaji huduma hiyo.

Madhara ya kuvaa viatu bila soksi
Trump augomea mkataba wa NAFTA