Serikali imesema kuwa itawachukulia hatua wale wote watakaobainika kuhusika katika kuvujisha mtihani wa kitaaluma wa mwaka wa pili wa matabibu pindi tu ripoti ya uchunguzi itakapokamilika na kuwasilishwa.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima, leo Octoba 27, 2021 wakati akifungua mkutano wa kujadili taarifa ya tathimini ya utoaji huduma za tabibu za kifamasia.

Serikali imeunda kamati ya uchunguzi iliyoshirikisha vyombo vyote, wakiwemo polisi na vyombo vyote vingine vinavyohusika na kuchunguza tuhuma kama hizi, ripoti ipo hatua za mwisho kukamilika, itasomwa wazi, maana wahalifu hao walichokitafuta watakipata“, amesema Dkt. Gwajima.

Serikali kupitia Wizara ya Afya itachukua hatua hizo kwa kufuata sheria, kanuni na miongozo bila kuonea yoyote ili iwe fundisho kwa wengine wanaofanya vitendo hivyo ambavyo ni kinyume na taratibu na sheria  za nchi.

Twiga Stars wadaka donge Nono
Familia ya kushangaza watoto wenye herufi za kufanana