Wamiliki wa Kampuni za Michezo ya kubahatisha nchini wametakiwa kujitokeza kwa wingi na kusaidia ukuaji wa sekta ya Michezo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe alipokutana na viongozi wa makampuni mbalimbali ya michezo ya kubahatisha nchini, ambapo amesema kuwa ili kuweza kukuza sekta ya michezo kwa maendeleo ya taifa ni lazima wajitokeze kwa wingi kama inavyofanyika katika mataifa mengine.

‘’Najua nyinyi ni wadau wakubwa wa michezo japo mchezo huu wa kubahatisha ni mgeni katika taifa letu ila ni mchezo unaokua kwa kasi hivyo ningependa kuona mnatoa ushirikiano katika kukuza sekta ya michezo kwa taifa kwani sekta hii imekuwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa fedha na miundombinu,’’amesema Dkt. Mwakyembe

Aidha, Dkt. Mwakyembe ametumia nafasi hiyo kuishukuru na kuipongeza Kampuni ya Mchezo wa kubahatisha ya Sportpesa kwa kutoa ufadhili wa kufanya matengenezo ya nyasi za uwanja wa Taifa zilizokuwa zimechakaa kufuatia maandalizi ya mashindano ya AFCON U17 ya 2019 yatakayofanyika nchini.

Hata hivyo, kwa upande wake Mwenyekiti wa Shirikisho la waendesha Michezo ya Kubahatisha (TSBA), Dhiresh Kaba ameishukuru serikli kwa kuwapatia nafasi ya kuchangia katika maendeleo ya michezo nchini.

‘

Magazeti ya Tanzania leo Novemba 25, 2017
Kafulila atua rasmi CCM