Serikali ya Tanzania imetambulisha tozo mpya ya kiasi cha Shilingi Milioni 2,106,170 sawa na Dola za Kimarekani $930 kwa wote wanaotaka kuendesha blogu za mtandaoni, hatua inayoleta mkakati mpya wa kuhakikisha Serikali inakuwa na mamlaka makubwa kwa vyombo hivyo.

Matakwa hayo mapya ya Serikali yanawataka wamiliki wote wa blogu kulipia na kujisajili kabla ya kuanza kuchapisha au kuweka maudhui katika mitandao yao.

Hata hivyo, hatua hiyo haitawaathiri waendeshaji wa blogu pekee bali redio za mtandaoni, warushaji wa matangazo kwa njia ya mtandao, majukwaa ya mtandao, watumiaji wa mitandao ya kijamii na vituo vya kutolea huduma ya mtandao.

Arsenal yatinga nusu fainali Europa
DRC yagoma kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa