Waamuzi  kutoka nchini Gabon  watachezesha mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya timu ya Tanzania, Taifa Stars na Misri Juni 4, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Shirikisho la Soka Barani Afrika, CAF limewateau waamuzi hao, Eric Arnaud Otogo Castane
atakayepuliza filimbi.

Castane mwenye umri wa miaka 40 ni mmoja wa waamuzi wazoefu barani Afrika. Amechezesha fainali tatu za AFCON. Atasaidiwa na washika vibendera Theophile Vinga  na Serge Meye huku Mwamuzi wa akiba akiwa ni  Mbina Gauthier.

Raia wa Sudan,  Tarig Atta Salih atasimama kama kamisaa wa pambano hilo ambalo Tanzania inahitaji ushindi wa angalau mabao 3-0 kuweka hai matumaini ya kuipiku Misri na kufuzu fainali za AFCON zitakazoandaliwa nchini Gabon mwakani.

Tanzia: Mchekeshaji maarufu wa 'Vituko Show' afariki
Sakata La Kushuka Daraja, Coastal Union Wainyooshea Kidole TFF

Comments

comments