Asilimia kubwa ya wanachama wa klabu ya Simba SC usiku wa kuamkia leo walikamilisha amza ya kumpa kura za ndio aliyekua mgombea pekee wa nafasi ya mwenyekiti wa bodi ya ukurugenzi ya klabu hiyo Swedy Nkwabi.

Swedi alisalia pekee yake kwenye kinyang’anyiro cha nafasi mwenyekiti wa bodi ya ukurugenzi baada ya Mtemi Ramadhani kujitoa, siku chache kuelekea uchaguzi mkuu ambao ulifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere mjini Dar es Salaam.

Cha kushangaa zaidi, wanachama wa klabu ya Simba SC waliopiga kura jana, hawakuwapigia kura kwa wingi viongozi wote waliomaliza muda wao, Iddi Kajuna, Said Tuliy, Ally Suru na Jasmine Costa ambao walikuwa akiwania nafasi ya ujumbe wa bondi ya wakurugenzi.

Waliochaguliwa katika nafasi za Ujumbe ni Hussein Kitta Mlinga, Dk. Zawadi Ally Kadunda, Suleiman Haroub Said, Mwina Mohammed Kaduguda na Asha Ramadhani Baraka.

Wengine waliogombea nafasi za Ujumbe ni Mohamed Wandi, Abdallah Rashid Mgomba, Christopher Kabalika Mwansasu, Alfred Martin Elia, Juma Abbas Pinto, Hamisi Ramadhani Mkoma, Abubakari Zebo na Patrick Paul Rweyemamu.

Uchaguzi wa Simba SC umefuatia uongozi uliopita ulioingia madarakani juni 30, mwaka 2014 chini ya Rais, Evans Elieza Aveva, Makamu wa Rais, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ na Wajumbe Iddi Kajuna, Said Tully, Collins Frisch, Ally Suru na Jasmine Badour kumaliza muda wake.

Lakini Aveva na Kaburu hawakufanikiwa kumalizia muda wao madarakani, kufuatia kuwekwa rumande katika gereza la Keko tangu Juni 29, mwaka jana kwa tuhuma za kughushi nyaraka, kesi ambayo bado inaendelea katika Mahakama ya Kisutu mjini Dar es Salaam.

Na Julai 1, mwaka jana, Kamati ya Utendaji iliwateua Salum Abdallah ‘Try Again’ na Iddi Kajuna kukaimu nafasi za Aveva na Kaburu na hao ndiyo waliosimamia mchakato mzima wa mabadiliko ya klabu kuelekea uchaguzi huo.

Nkwabi ambaye amekidhi matakwa ya Katiba mpya ya Simba SC kuwa na elimu ya Shahada sasa ataongoza Bodi ya Wakurugenzi itakayokuwa na Wajumbe wanane chini yake huku akiwa na mamlaka ya kuteua Wajumbe wengine wanne, kati yao mmoja lazima awe mwanamke ili kukamilisha Bodi ya Ukurugenzi ya watu wanane.

LIVE: Msemaji wa Serikali akizungumza na waandishi wa habari
Lionel Messi kuikabili Inter Milan

Comments

comments