Baadhi ya Mashabiki wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Simba SC, wameongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam na kuweka wazi msimamo wao.

Wanachama hao wamezungumza baada ya aliyekua Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu ya Simba SC Haji Manara kuchafua hali ya hewa jana Jumatano (Agosti 04).

Kwa pamoja wanachama hao wamesema wako pamoja na Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu hiyo, na ikitokea mtu akatoboa mtumbwi wao lazima watamshughulikia.

Wamesema hawajawahi kumpenda mtu na hawatakuja kupenda mtu, zaidi ya kutanguliza mbele mapenzi na klabu yao, na watailinda kwa gharama yoyote.

“Sisi kama mashabiki tuko pamoja na viongozi wetu na tunaimani nao, tunawaomba TU wasajili wachezaji Bora na wazuri na tunawaahidi kuwa siku ya Simba day tutaujaza uwanja maradufu zaidi ya siku zingine zote hatuwezi kuyumbishwa na mtu 1 anae isema Simba vibaya” wamesema Mashabiki wa Simba SC

Pia wamesema mti ukiivisha matunda siku zote huwezi kuukata, hivyo wataendelea kutoa sapoti yao yote kwa mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC Mo Dewji.

Dili: Wanaopata chanjo ya corona kulipwa Sh. 2,300,000
Chama: Ligi Kuu itakua ya 'MOTO' msimu ujao