Wanadiplomasia 35 wa Urusi waliofukuzwa nchini Marekani na Rais wa nchi hiyo Barrack Obama, kwa tuhuma za udukuzi kwenye uchaguzi mkuu wa rais, leo wameondoka rasmi kurejea nchini mwao.

Aidha,Vyombo vya habari vya Urusi vimeripoti kuwa wanadiplomasi hao wameondoka  kwa ndege maalumu iliyotumwa na Serikali ya nchi hiyo.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Urusi kushutumiwa kuwa ilijaribu kuingilia uchaguzi wa Urais nchini Marekani kupitia mtandaoni.

Vyombo vya kijasusi vya Marekani vinadai kuwa utawala wa Urusi ndio ulioamuru kudukuliwa  hasa tovuti ya chama cha Democratic ili kuvuruga kampeni za Clinton na kumsaidia Donald Trump ambae sasa ndiye rais mteule.

Kocha Salum Mayanga Arudishwa Taifa Stars
Mourinho: Sijafurahishwa na kuondoka kwa Erick Bailey