Serikali ya Nigeria kwa ushirikiano na shule  iliovamiwa na wanamgambo wa Boko Haramu imethibitisha kukosekana kwa wanafunzi wa kike wapatao 111 baada ya  shambulizi la wanamgambo wa kundi la Boko Haramu .

Shambulizi hilo la Boko Haramu lilitokea wiki iliyopita katika eneo la Yobe.

Kwa mujibu wa taarifa, wanafunzi wapatao 815 ndio waliorejea shuleni baada ya uvamizi na shambulizi la wanamgambo hao.

Ikumbukwe kuwa wanafunzi zaidi ya 276 wa Chibok walitekwa mwaka 2014 na wanamgambo wa kundi hilo la kigaidi nchini Nigeria.

Kundi la wanamgambo wa Boko Haramu lilianza harakati zake za kigaidi nchini Nigeria  mwanzoni mwa miaka ya 2000 likipambana na elimu ya Magharibi Afrika Magharibi.

 

Mambosasa: Huyu anafanya vitendo vya unyang'anyi kwa kutumia nguvu kwa wanawake
Zitto ataka hesabu ya wapinzani waliobaki