Jumla ya wasichana nane ambao ni wanafunzi wamegundulika kupata ujauzito katika kipindi cha Januari hadi mei mwaka huu katika wilaya ya Makete mkoani Njombe.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Makete Mh Veronica Kessy wakati akitoa hotuba yake katika baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Makete hivi karibuni

Mkuu huyo amesema suala hilo linaichafua wilaya ya Makete hivyo kuomba ushirikiano kutoka kwa madiwani hao katika mapambano dhidi ya vitendo hivyo vinavyokatisha safari ya mafanikio ya wanafunzi wa kike

“swala ambalo linatuchafua katika wilaya yetu ni swala la ulinzi kwa maana ya wanafunzi wetu wa kike kupata ujauzito,sisi kama kamati ya ulinzi na usalama tunaliona kwamba hili tusipoliwekea mikakati maalumu bado litakuwa sio kusudi letu maalumu,kwa kuwa hivi tunavyoongea tayari wanafunzi 8 wamepatikana na ujauzito shuleni,niombe sana tusimamie maswala haya na tuweke hata mikakati ya kuona namna gani tunawatega wale ambao wanakuwa wasumbufu kwa watoto wakike”alisema Veronica Kessy.

Daniel Okoka ni Diwani wa kata ya Lupila akichangia suala hilo amesema bado kumekuwa na ulegevu katika kupambana na makosa ya watuhumiwa wanaowapa ujauzito wanafunzi

“Kwenye eneo hili sidhani kama vyombo vinavyohusika tunaungana kwa pamoja kwenye mapambano ya jambo hili ninao mfano hai kwenye kata yangu ya lupila tunakamata mpaka watuhumiwa mpaka tuwapeleka polisi lakini yapo maswala madogo madogo yanayofanywa wahusika wasishughulikiwe kwa wakati”alisema Okoka

Godfrey Gogadi ni mwanasheria wa halmashauri ya wilaya ya Makete amezungumzia changamoto iliyopo kuhusiana na hoja iliyotolewa na Diwani Okoka

“kuna changamoto ya makubaliano au kuficha taarifa lakini pia kuna changamoto ya wazazi kubadilisha zile kauli na ukifuatilia zaidi jamii au familia husika zinashirikiana katika kumbadilisha mtoto kwa hiyo swala hili sio la mtu mmoja hata tukisema tuiachie polisi haiwezi”alisema Gogadi

Imamu mkuu Ghana amesherekea siku yake ya kuzaliwa akiwa Kanisa Katoliki
Usafiri wa ndege waendelea kutia wasiwasi