Serikali nchini, imesema itaweka mkakati wa kuwatumia Wanafunzi wanaosoma kozi za Afya Vyuo vya kati na Vyuo Vikuu kutoa Elimu ya Afya katika Shule za Msingi, Sekondari na ngazi ya jamii, ili kuhakikisha elimu hiyo inafika Shuleni kwa ufasaha.

Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya ELimu ya Afya kwa Umma, Idara ya Kinga, Wizara ya Afya, Dkt. Tumaini Haonga ameyasema hayo katika Warsha ya siku mbili ya “Afya Day” iliyofanyika Chuo Kikuu Cha Mtakatifu Yohane jijini Dodoma.

Amesema, “mwanafunzi wa chuo kikuu anayesoma ngazi ya Astashahada, Stashahada na Shahada kwenye eneo la afya muda wa kufanya mazoezi ni muhimu, kinachotakiwa ni kuainisha vipaumbele na kufanya mawasiliano na uongozi wa vyuo kwani kuna changamoto nyingi kwa vijana ikiwemo masuala ya lishe na afya uzazi.“

Awali, Afisa Mpango wa Afya shuleni ,Elimu ya Afya kwa Umma ,Idara ya Kinga,Wizara ya Afya, Magdalena Dinawi amesema kwa taratibu za nchi kijana anaweza kupima Virusi vya UKIMWI kuanzia miaka 15 na kuendelea bila ridhaa ya wazazi wake.

Rais Samia aongoza kikao cha Baraza la Mawaziri
Mwanasiasa maarufu auawa kwa risasi na wasiojulikana