Jeshi la Polisi jijini Bujumbura nchini Burundi limewatia nguvuni kundi kubwa la wanafunzi na kuwashtaki wanaotuhumiwa kuharibu picha ya Rais Pierre Nkurunzinza.

Wanafunzi hao wamekamatwa katika operesheni muhimu baada ya kukithiri kwa vitendo vya wanafunzi kutoa matusi na kuharibu picha ya Mkuu wa Nchi kinyume cha Sheria.

Kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo, kuharibu picha ya Rais ni kosa kisheria na mtu anaweza kukabiliwa na kifungo hadi cha miaka 10 jela.

Taarifa zimeeleza kuwa Polisi wamekuwa wakipambana na makundi ya wanafunzi wanaoandamana katika jiji hilo wakipinga Serikali hiyo. Kwa mujibu wa BBC, jana Polisi walifyatua risasi angani na mabomu ya machozi kutawanya makundi ya wanafunzi waliokuwa wakiandamana.

Jose Mourinho Apongezwa Kwa Mipango Ya Usajili Wa Bailly
Museveni amteua Mkewe kuwa Waziri