Wakazi Mkoani Njombe wametakiwa kuendeleza juhudi za Upandaji miti ya Matunda ili kuhakikisha mazingira ya mkoa huo yanakuwa ya kuvutia ili kuepusha athari zitokanazo na Uharibifu wa Mazingira.

Hayo yamesemwa na Wanafunzi kutoka chuo cha Dublin Business School kutoka nchini Ireland walioambatana na Mtanzania, David Nyaluke anayefundisha katika chuo hicho mara baada ya kutembelea katika chuo cha Amani kilichopo mkoani Njombe.

Wakizungumza wakati wa zoezi la kupanda Miti 200 ya matunda ya Parachichi na Vivuli nje ya majengo mapya ya chuo cha Amani yaliyopo eneo la Nyekamtwe mjini Njombe Wanafunzi hao wamesema kuwa kutokana na kupotea kwa uoto wa asili katika nchi nyingi Duniani hivyo zoezi la upandaji miti linatakiwa kuwa endelevu.

Kwa upande wake Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Amani kilichopo mkoani Njombe, Emmanuel Mlelwa pamoja na Rais wa Chuo cha Dublin kutoka nchini Ireland, James Barke wamesema kuwa zoezi hilo la upandaji miti ni ishara ya kuwaunga mkono wakazi wa mkoa wa Njombe kwa masilahi ya Taifa.

Baadhi ya wakufunzi kutoka chuo cha amani mjini Njombe wamesema kuwa wataendeleza uhifadhi wa Mazingira pamoja na kuendeleza ushirikiano mwema kati yao na chuo cha Dublin Business School kutoka nchini Ireland.

Waziri Jafo kushughulikia tatizo la VAT kwa wakandarasi
DC Kassinge aonya kuhusu mifuko ya rambo, ' tukikukamata utapata tabu sana'