Wanafunzi waliosoma shule binafsi na wale waliosoma diploma na kufanya mitihani wakiwa watahiniwa wa kujitegemea wamenyimwa mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya elimu ya juu (HESLB), ambapo hali hiyo imesababisha wanafunzi wengi waliokuwa vyuoni kuanza kurejea makwao  kutokana na kushindwa kumudu gharama.

Hayo yamesemwa na mkurugenzi mtendaji wa HESLB Abdul Razaq Badru, amesema mpaka sasa wametoa mikopo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza 20,183 kati ya 25,717 watakao nufaika na mikopo,na kuongeza kuwa wanafunzi wengi waliokosa mikopo ni wale waliosoma shule binafsi sababu kubwa ikiwa ni taarifa za nyuma ndiyo chanzo cha kukosa mikopo.

Ameongeza kuwa si wote waliosoma shule binafsi wanauwezo ndiyo maana wamefungua dirisha la kukata rufani na kuongeza kuwa inawezekana wakati wa ujazaji fomu kulikuwa na makosa na wanatakiwa kupeleka barua na vielelezo ili waweze kupata mikopo.

Aidha, Badru alivitaja vigezo vilivyowekwa na serikali kwa wanafunzi watakaopata mikopo ni Yatima , Walemavu, wanafunzi wanaotoka familia zenye hali duni ya kimaisha hususani waliosoma shule za umma, na kuongeza kuwa vipa umbele vya kitaifa ni vile vinavyoendana na mpango wa maendeleo wa taifa wa miaka mitano Dira ya Taifa ya maendeleo 2025 na mafunzo ambayo yatazalisha wataalam.

Hata hivyo Badru alizitaja fani hizo kuwa ni Sayansi za Tiba na Afya, Ualimu wa Sayansi na Hisabati, Uhandisi wa Viwanda, Kilimo, Mifugo, Mafuta na Gesi Asilia, Sayansi Asilia na Sayansi za Ardhi,usanifu majengo na miundo mbinu.

 

Magufuli avunja rekodi ya Lowassa, amfunika
GGM yakabidhi madawati yenye thamani ya mil. 750