Wanafunzi 316 wa Chuo Kikuu cha St. Joseph waliokuwa wakisoma Kozi Maalumu ya Shahada ya Elimu ya Hesabu na Sayansi ya kabla ya kusimamishwa hivi karibuni, wamekubaliwa kufungua kesi dhidi ya Chuo hicho na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, jana iliridhia maombi ya wanafunzi wanne, Ramadhani Kimenya, Faith Kyando, Oswald Mwinuka na Innocent Peter kuwa wakilishi wa wanafunzi wenzao katika kesi hiyo.

Katika kesi ya msingi, wanafunzi hao wanaiomba Mahakama kuagiza Chuo Kikuu cha St. Joseph pamoja na TCU kuwalipa fidia ya miaka mitatu waliyotumia kusoma katika chuo hicho.

Uamuzi huo kuwaruhusu kufungua kesi uliotolewa na Jaji Elieza Feleshi, uliridhiwa na mawakili wa Chuo cha St Joseph, Jerome Msemwa na wale wa TCU, Rose Rutta na Judith Misokia

Wanafunzi hao wametaka masomo yasimamishwe hadi kesi hiyo itakapomalizika na Mahakama kutoa uamuzi wake.

Kusimamishwa kwa wanafunzi hao kulitokana na athari iliyotokana na agizo la Serikali kuwaondoa katika Chuo Kikuu cha Dodoma wanafunzi zaidi ya 7000 waliokuwa wakisoma kozi maalum ya Shahada ya Sayansi na Hesabu.

 

Habari Mpasuko: Magufuli afanya mabadiliko Baraza la Mawaziri
Video: Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amedaiwa kuonyesha alama ya dole bungeni, Naibu spika ametoa mwongozo