Wanafunzi wawili wa wanaosoma Chuo Kikuu wamezama katika Mto Yala ulioko Bondo, Kaunti ya Siaya nchini Kenya Jumamosi jioni.

Kwa mujibu wa ripoti ya polisi wa eneo hilo iliyokaririwa na Citizen, Derick Auka ambaye alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Chuo Kikuu Cha Jaramogi Oginga Odinga na rafiki yake wa kike Sharon Atieno ambaye ni mwanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi ngazi ya shahada, walikumbwa na janga hilo walipokuwa wanatembea na kujipiga picha (selfie) kandokando ya maporomoko ya mto huo, kwenye daraja la Got-Winyo.

Taarifa ya Mamlaka ya Mji wa Bondo imeeleza kuwa Shalon alitereza na kuangukia mtoni alipokuwa anatembea akijipiga picha kando ya mto na kwamba Auka alizama pia alipokuwa akijaribu kumuokoa rafiki yake huyo wa kike.

Mkuu wa Polisi wa Bondo, Harriet Kinya alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa wameanza msako kuwatafuta wawili hao wakati jeshi hilo likiendelea na upelelezi.

Kinya alitoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari wanapokuwa kwenye shughuli zao za kila siku kando kando ya mto hususan katika kipindi hiki cha mvua.

Vyuma vya reli (SGR) vilivyoibwa vyakutwa kwa Diwani
LIVE: Rais Magufuli akihutubia maadhimisho ya miaka 150 ya Uinjilishaji Tanzania