Wanafunzi zaidi 210 katika shule ya msingi Nyanyati Mkoani Mtwara wanapata elimu yao chini ya mti kutokana na kukosa madarasa na madawati.

Mwalimu mkuu Shule hiyo, Shaibu Hoja alisema kuwa shule hiyo ambayo ilianzishwa miaka mitatu iliyopita ina darasa moja tu la kusomea huku kukiwa na walimu wawili pekee walioajiriwa na serikali na mwalimu mmoja wa kujitolea anaefanya kazi kwa muda mfupi.

Mwalimu Hoja aliongeza kuwa pamoja na changamoto hizo, bado kuna tatizo kubwa la ukosefu wa vifaa vya kufundishia pamoja na nyumba za walimu hivyo kuwafanya walimu hao wachache kushindwa kuwatosheleza wanafunzi hao kitaaluma.

Alisema kuwa nyakati za mvua wanafunzi hulazimika kubaki majumbani kwa kuwa hawawezi kuendelea kusomea chini ya mti huo.

“Changamoto ya kutokuwa na mdarasa ni kubwa sana kwa sababu wanafunzi wanapata shida zaidi wakati wa mvua,” Mwalimu Hoja alimwambia mwandishi wa The Citizen.

Hivi karibuni, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Joyce Ndalichapo alikiri kuwa wanafunzi hawawezi kupata elimu bora katika mazingira hayo duni. Alisema watendaji katika ngazi za Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa wanaoshughulikia masuala ya elimu wameshaagizwa kuhakikisha kuna mazingira bora ya utoaji wa elimu ikiwa ni pamoja na vifaa vya kufundishia.

 

 

Mabalozi wa Iran watimuliwa Katika nchi Hizi
Hizi ni picha Tano zilizopendwa zaidi mwaka 2015