Wananchi wa kata ya Kitandililo Halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe, wameazimia kuwa mzazi au mlezi atakae mshawishi mwanae afanye vibaya katika masomo yake hususani katika mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi hatua za Kisheria zichukuliwe dhidi yake.
Licha ya kuamua mzazi huyo ashughulikiwe kisheria pia wananchi hao wamekubaliana kuwa muhusika apewe adhabu ya kumsomesha mtoto wake katika Shule ya Sekondari Mtwango ambayo ni shule binafsi, ili kukabiliana na gharama zilizopo katika Shule hiyo tofauti na Shule za Serikali.
Wananchi hao mbele ya Diwani wa Kata ya Kitandililo, Imani Fute wamekubaliana kuwa mtu yeyote atakaye onekana amesimama na mwanafunzi wa kike kwa zaidi ya dakika tano atakabiliwa na adhabu ya kununua mifuko 10 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa mabweni katika shule ya Sekondari ya kata hiyo.
“Ukimpenda Mwanafunzi ukubali kuchangia mifuko kumi ya saruji ili ajengewe mabweni apate kusoma kiurahisi zaidi kwa kutokutembea umbali mrefu”. Wameeleza Wananchi hao.
Diwani wa Kata ya Kitandililo, Imani Fute amesema kuwa wameamua kuchukua maamuzi hayo baada ya kubaini uwepo wa wazazi wanao washawishi watoto wao kufanya vibaya katika mtihani yao, licha ya kuwa na uwezo mzuri darasani, Pamoja na kuzuia tatizo la mimba Shuleni kwa kuwa hadi sasa Tayari wanafunzi wa kike wanne wamepata ujauzito.

Wanawake Kigoma wapigwa faini kwa kujifungulia nyumbani
Video: Masele akalishwa kiti moto Dodoma, Korosho zawa moto bungeni