Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme leo Februari 13, 2020 amehudhuria mazishi ya miili ya wanafunzi watano waliofariki dunia mara baada ya kugongwa na gari katika ajali iliyosababishwa na uzembe wa dereva.

Mazishi hayo yamefanyika katika makaburi ya kijiji cha Ndelenyuma halmashauri ya Madaba mkoani Ruvuma.

Wanafunzi hao watano wa shule ya msingi Ndelenyuma, walifariki dunia katika ajali iliyotokea Februari 12, 2020 baada ya kugongwa na gari aina ya Land Cruiser lililokuwa likitokea Songea kwenda Madaba.

Ambapo gari hilo liliacha njia na kuwagonga wanafunzi kisha likapinduka, mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo dereva aliyefahamika kwa jina moja la Saalum alaamua kutoroka na kukimbia katika eneo hilo la tukio.

“Chanzo cha ajali iliyoua wanafunzi watano ni mwendo kasi wa Dereva wa Land Cruiser, hakujali mvua na utelezi, Gari likamshinda na kuwagonga Watoto pembezoni mwa Barabara wakadondokea mtaroni, watatu walisombwa na maji miili yao imekutwa Mita 100 kutoka eneo la ajali” amesema Simon Maigwa, RPC Ruvuma.

Aidha dereva huyo kwa uzembe amekatisha ndoto za malaika hao watano wasio na hatia, Mungu azipumzishe roho za marehemo hao mahali pema peponi.

Dar24 inatoa pole kwa ndugu jamaa na marafiki wote walioondokewa na wapendwa hao ghafla.

Mwanamke aliyejaribu kufungua mlango wa ndege ikiwa angani atupwa jela
Angalia orodha ya waliopelekwa kamati ya nidhamu TFF