Zaidi ya wanafunzi 50 wa kidato cha kwanza (C) wanaosoma katika Shule ya Sekondari Mingoyo Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Mkoani Lindi wamelazimika kutumia maabara ya Phizikia kama Darasa kufuatia changamoto ya madarasa iliyopo shuleni hapo.
 
Wakizungumza na Dar24 Media baadhi ya wanafunzi hao akiwemo, Marijani Hamisi, Mwajuma Adam na Khalphan Jamary wamesema kuwa changamoto wanayokutana nayo wakiwa wanatumia madarasa hayo kuwa wanalazimika kuhama hama mara kadhaa katika darasa lao pindi darasa hilo likitakiwa kutumiwa na wanafunzi wengine kwa ajili ya kujifunza kwa vitendo.
 
”Tunatumia darasa hili kutokana na changamoto ya madarasa iliyopo shuleni kwetu lakini hata hivyo mara nyingine kama wanafunzi wa darasa lingine wanataka kufanya practical sisi tunalazimika kuhama na kuhamia darasa lingine hivyo inatuletea usumbufu na wakati mwingine tunapoteza muda wa kujisomea kwa kutuhamisha hamisha,”amesema Marijani Hamisi ambaye ni miongoni mwa wanafunzi hao
 
Aidha, kufuatia changamoto ya Madarasa iliyopo katika Shule hiyo Serikali imetoa kiasi cha shilingi. Milioni 37.5 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa vyumba vitatu vya Madarasa katika Shule hiyo hali iliyomfanya mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi kutembelea Shuleni hapo na kuona Maendeleo ya ujenzi wa madarasa hayo na kuonyesha kurizishwa na ujenzi huo.
 
Awali akitoa taarifa ya Shule hiyo Mkuu wa Shule ya Sekondari Mingoyo, Mwichande Lihoma amesema kuwa Shule hiyo kwa sasa inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa vyumba 7 vya madarasa huku akisema kuwa ujenzi wa Madarasa hayo matatu utasaidia kupunguza changamoto hiyo nasasa kufanya upungufu wa vyumba vinne 4 vya madarasa.

Azam yapewa leseni kuanza kuonesha chaneli za ndani bure
Rais Magufuli afanya uteuzi mwingine UDOM