Watu wenye silaha wamevamia chuo kimoja katika jimbo la Kaduna nchini Nigeria, na kuteka nyara idadi kubwa ya Wanafunzi.

Uongozi wa jimbo hilo la Kaduna umesema kuwa, wengi wa Wanafunzi waliotekwa nyara ni wa Kike.

Mpaka sasa haijafahamika ni watu ama kikundi gani lilichofanya tukio hilo katika chuo hicho cha misitu, ambacho kipo karibu na chuo cha mafunzo ya kijeshi.

Kwa sasa uongozi wa chuo hicho unaendelea kufuatilia taarifa mbalimbali ili kufahamu ni Wanafunzi wangapi walikuwepo chuoni wakati tukio hilo linatokea.

Kavazovic anukia Jangwani
Kim Poulsen azidisha mbinu Taifa Stars