Wanajeshi wanne nchini Somalia wameuawa na wengine sita kujeruhiwa vibaya na mtu mmoja aliyejitoa mhanga katika mgahawa mmoja wa chai uliopo katika mji wa Galkayo nchini humo.

Kijana mmoja aliyevalia koti lenye mabomu aliingia ndani ya mgahawa huo mahala ambako wanajeshi wa serikali ya Somalia walikuwa wamekusanyika.

Aidha, hakuna mtu yeyote aliyejitokeza kuhusika kwa shambulizi hilo lakini lilionekana kuwa ni shambulizi lililofanywa na kundi la wanamgambo wa Al-Shabaab.

Hata hivyo, kundi la wanamgambo la Al- Shabaab limekuwa likishambulia maeneo mbalimbali ya serikali, hivyo kuhusishwa moja kwa moja na shambulizi hilo.

 

Askofu Malasusa na wengine 2 watengwa na kanisa la KKKT
Korea Kaskazini yakubali kusitisha mpango wake wa nyuklia

Comments

comments