Kutokana na kuwepo kwa matukio mbalimbali yanayo tishia uhai wa vijana, ambayo yanahusishwa na imani za kishirikina katika kijiji cha Namasalau Mkoani Ruvuma, baadhi ya wananchi waishio hapo wameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kuwapelekea mganga wa jadi ili aweze kusaidia kuwabaini wanaohusishwa na uchawi.

Wakitoa kilio chao katika mkutano wa hadhara mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Juma Homera alipofanya ziara ya kuwatembelea wananchi hao baada ya kusikia taarifa za kuongezeka kwa vifo vya watu katika mazingira na matukio ya kutatanisha.

Wananchi waliopoteza maisha kwa sababu zinazodaiwa ni zakutatanisha ni Mnjaid Mohamed, Ziada Athumani na Awetu Sandali ambao wote walifariki mwezi octoba mwaka huu, na wengine wawili wamenusurika kifo  kwa kuuguaa.

Akijibu maombi hayo, Homera alisema kuwa kwavile serikali haiamini mambo ya kishirikina anaandaa utaratibu wa kwenda kukutana na wazee wa kijiji ili kutafuta mustakabali wa kumaliza tatizo hilo na kumtaka Diwani wa kata hiyo, Khadija Timamu kusimamia maandalizi ya kikao hicho ili kiweze kufanyika mapema.

 

 

 

 

Upasuaji wa Hawa wamalizaka, madaktari wamtabiria haya
Marcos Alonso akata ngebe za Real Madrid