Wakazi wa kijiji cha Igalako kata ya Mahongole wilayani Mbarali mkoani Mbeya wameandamana kupinga agizo la serikali la kutaka kuwaondoa kwa nguvu waganga wa kienyeji wanaojulikana kama Lambalamba kijijini hapo kwa madai ya kwamba wanawasaidia kusafisha nyota na kuwaondolea nuksi kwenye familia zao na kuwaepusha na matukio ya kichawi yanayoendelea kijini hapo.

Wananchi wamesema kuwa haiwezekani kuwaondoa Lambalamba/waganga wa kienjeji kwasababu tangu waanze kufanya kazi yao uchawi umepungua sana kijijini hapo.

”Watoto usiku hawalali, hata sisi watu wazima mimi kuna siku nimelala nimeamkia juu ya kaburi lakini lambalamba wakasafisha sasa mnawakatalia nini? amehoji mmoja wa wanakijiji.

Aidha Mwakilishi Mkuu Wilaya ya Mbarali, Rashid Ngovano amesema hilo swala wanalotaka wananchi haliwezekaniki amewataka lambalamba wafike kwenye ofisi husika kitengo cha tiba asili ili waweze kujisali na kuhalalisha kazi yao.

Hata hivyo moja ya mwananchi amehoji kuwa Serikali haijui wala haiamini juu ya uchawi hivyo ameomba iwaachie huru kwani wananchi ndio wanaojua uchawi na ndio wanaodhurika na uchawi wamedai wanawahitaji sana Lambalamba ili kukomesha matukio ya kichawi kijijini hapo.

Video: Mgongolwa afafanua kuhusu misamaha ya JPM kwa wafungwa
Video: TRA yatishia kuuza mali za Paul Makonda, Bajeti kilimo kaa la moto