Wanajeshi wamezima shambulizi kutoka kwa kundi la al-Shabab kaunti ya Lamu nchini Kenya, ambapo wanamgambo wanne waliuawa na silaha kadha kupatikana wakati wa ufyatulianaji huo wa risasi.

Wanajeshi wamekuwa wakiwawinda wanamgambo wa al-shabab baada ya kafanya shambulizi dhidi ya KDF eneo Mangai jana jioni.

Gruneti, bunduki nne aina ya AK47 na vilipuzi vilipatikana.

Jaribio hilo la shambulizi lilifanyika karibu na kijiji cha Baure kilicho umbali wa kilomita 60 kaskazini mwa mji wa pwani mwa Kenya wa Lamu.

Yamekua ni matukio mfululizo ya mashambulizi yanayofanywa na wanamgambo wa kundi la Al shabaab kueleke Nchini Kenya.

Tundu Lissu alala Rumande, adaiwa kutoa maneno mengine ya uchochezi
Ukawa Waeleza Nia ya Kwenda ICC