Jeshi la polisi nchini Uganda limesema kuwa limepokea taarifa 48 za watu kutoweka na kuingizwa katika biashara haramu ya  binadamu nchini humo kwa kipindi cha miezi sita iliyopita.

Hata hivyo, inaaminiwa kuwa watu 121 wamehusishwa katika biashara hiyo na inaripotiwa kuwa watu 78 walisafirishwa nje ya nchi kibiashara na watu wasiojulikana toka mataifa ya mashariki ya kati na huku wengine 43 wakitoweka kaatika mazingira ya kutatanisha nchini humo.

Polisi wamesema wamefanikiwa kuwaokoa watu hao waliotoweka katika mazingira ya kutatanisha .

Moses Binoga kutoka kitengo kinachoshughulikia matukio ya watu kupotea amesema idadi kubwa ya watu waliotoweka na kupatikana ni wasichana.

Wasichana wengi waliohojiwa wamekuwa wakilalamika  wananyanyaswa kingono wanapopelekwa huko katika mataifa ya Mashariki ya kati.

Justin Bieber awakera mashabiki wimbo wa Despacito
Wenger afunguka kuhusu sakata la kumuweka sokoni Sanchez