Serikali ya Tanzania kupitia Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi (Green Climate Fund) imepata fedha za kutekeleza mradi mkubwa wa maji kutoka Ziwa Victoria hadi Mkoa wa Simiyu ambapo fedha za Mradi huo zitapitia Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW).

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora wakati wa kikao kazi kilichojumuisha wadau wanaohusika na utekelezaji wa Mradi wa maji kutoka mkoani Simiyu.

Amesema kuwa fedha hizo zinapitia Benki ya Maendeleo ya Ujerumani kwakuwa Serikali ya Ujerumani imekua ikifadhili miradi mbalimbali ya maji hapa nchini hivyo imependekezwa kwa fedha hizo kupitia katika Benki hiyo.

Prof. Kamuzora ameongeza kuwa huu ni mradi mkubwa sana na wenye manufaa kwa wakazi wa Simiyu ambapo Mfuko wa Mabadiliko ya tabianchi umetoa kiasi cha 102,700,000 EURO, Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW) itachangia 25,900,000 EURO na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itagharamia kiasi cha 13,100,000 EURO. Vilevile jamii inayozunguka mradihuo  itachangia kiasi cha 1,500,000EURO, hivyo mradi wote unatarajiwa kugharimu kiasi cha EURO 143,000,000 na utatekelezwa ndani ya kipindi cha miaka mitano.

Aidha, kwa upande wake Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Mabadiliko ya Tabia Nchi anayeiwakilisha Afrika. Richard Muyungi, amesema kuwa ni mradi mkubwa sana na wa kwanza duniani kupatiwa fedha kupitia mfuko huo ambazo si mkopo.

Hata hivyo, Kikao cha Wadau  cha kujadili utekelezaji wa Mradi wa maji wa Simiyu, kimeratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais ambao ni Wasimamizi wa Fedha za Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi hapa nchini na wanadhamana ya kuhakikisaha fedha za Mfuko huo zinatumika ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuendana na mipango ya nchi iliyojiwekea

Mrisho Mpoto kuliamsha ‘dude’ na Kassim Mganga, sasa ni Kitendawili
Mbowe amjibu Polepole kuhusu kigogo wa Chadema anayetarajiwa kuhamia CCM