Wakulima Mkoani Njombe wameshauliwa kuweka akiba ya chakula cha kutosha ili kuondokana na Baa la njaa wanaloweza kukumbana nalo mara baada ya kuuza mazao yao kwa walanguzi wakifurahia fedha ya muda mfupi.

Ushauri huo umetolewa na Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM, Edward Mwalongo wakati akizungumza na Wananchi katika Vijiji vya Kata ya Luponde halmashauri ya Mji wa Njombe.

Amesema kuwa katika kipindi hiki cha mavuno baadhi ya Wakulima huwa na tabia ya kuuza mazao bila kuweka akiba majumbani, jambo ambalo linahatarisha usalama wa familia kutokana na kukosa chakula.

“Wananchi katika kipindi hiki cha mavuno baadhi yetu huwa na tabia ya kuuza mazao yetu bila kuweka akiba ya chakula majumbani kisa fedha kidogo tunazopata kwa Walanguzi, naomba sana tuwe makini juu ya hili maana baadhi ya Mikoa hapa Nchini Inashida ya Chakula,”amesema Mwalongo

Kwa upande wake bwanashamba wa halmashauri ya mji wa Njombe, Nolasco Kilumile amesema kuwa licha ya kufanyabiashara, Wakulima wanatakiwa kuweka akiba ya Chakula kwaajili ya Familia zao pasipo kuingia Tamaa ya Fedha na kusahau majukumu yao katika Familia.

Imeelezwa kuwa Mkoa wa Njombe umeendelea kuongoza katika Tatizo la Udumavu Kitaifa, hivyo Jamii ya Mkoa huo inashauriwa kutumia Mboga za majani, Matunda na Vyakula mchanganyiko vinavyozalishwa katika Mkoa huo ili kutokomeza tatizo la Udumavu.

Video: Simu ya Magufuli kwa Uhuru yaibua mazito, Ofisa mbaroni kwa rushwa ya mbuzi 10
Video: Waandishi wa habari acheni kuchokonoa chokonoa, mtatuharibia- Warrace Karia