Wakazi wa kata ya Rulenge kwa kushirikiana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ngara mkoani Kagera wamejenga madarasa ya shule ya msingi Murugalagala ili kupunguza adha ya wanafunzi kusongamana katika chumba kimoja.

Hayo yamesemwa na Katibu wa CCM wilaya ya Ngara, John Melele wakati wa ujenzi huo ambapo amesema kuwa viongozi na wanajamii wameungana kuonyesha mshikamano na kuguswa na changamoto za shule hiyo katika utoaji wa taaluma.

Amesema kuwa ametoa mifuko mitatu ya saruji na kuchangia fedha taslimu shilingi elfu 40 na kuahidi mifuko mingine mitatu iii kuweza kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa hayo.

Aidha, amewaonya viongozi wa CCM wilayani Ngara wanaoendekeza malumbano na kujenga matabaka na ukanda badala ya kuwa na umoja wakaandaa wanachama wenye sifa watakaoshiriki uchaguzi wa serikali za mitaa na kuchochea maendeleo.

“Sitamuacha mwanachama yeyote mwenye sifa ya kugombea bila kuangalia anatoka ukanda gani, masikini au tajiri hata kama ni mpya kutoka upinzani atapitishwa ilimradi nisivunje katiba ya chama hiki,” amesema Melele

 

 

CCM hata wakitawala milele mimi sina tatizo- Godbless Lema
Shonza aipa tano 'Tetema' ya Rayvany na Diamond

Comments

comments