Maelfu ya waandamanaji wanaounga mkono jeshi, nchini Sudan wamejitokeza mitaani kushinikiza kuvunjwa kwa serikali ya mpito kwa madai kwamba “imefeli ” kisiasa na kiuchumi.

Haya yamejiri wakati kuna mpasuko wa kisiasa Sudan kati ya vikundi vinavyoongoza mchakato wa mpito unaokumbwa na msukosuko, baada ya miongo miwili ya utawala wa mkono wa chuma wa rais wa zamani Omar al-Bashir, aliyeng’olewa madarakani na jeshi Aprili 2019.

Maandamano hayo yameandaliwa na kundi lililogawika la vuguvugu liitwalo FCC, ambalo lilihusika pakubwa kuandaa maandamano dhidi ya Bashir na pia kuwa mshirika mkubwa kwenye mchakato wa mpito

Waandamanaji wameishtumu serikali ya sasa kwa kushindwa kuleta haki na usawa na wanataka serikali itakayoongozwa na jeshi.

Waziri mkuu Abdallah Hamdok siku ya Ijumaa alionya kwamba serikali ya mpito inakumbwa na changamoto ngumu na hatari na wakosoaji wa serikali wamedai kwamba maandamano hayo yamehusisha wafuasi wa utawala wa zamani wa Bashir.

Tunataka Mawaziri wachapa kazi kama Aweso:Rais Samia
Mwanza kunufaika na Uongozi wa Rais Samia