Rais wa Marekani, Donald Trump amesema anaitaka Marekani “ifunguliwe tena” kabla ya sikukuu ya Pasaka (Aprili 12), licha ya onyo kuwa kufanya hivyo kutaleta hatari kubwa kwa juhudi za kudhibiti mlipuko wa virusi vya corona  nchini humo.

Kauli hiyo imekuja kufuatia majimbo 17 ya nchi hiyo kutoa amri kwa wakazi wake kukaa nyumbani kuanzia leo Machi 25, 2020.

Rais Trump amesema Serikali yake itatathmini upya maagizo ya kuepuka mikusanyiko kwa siku 15, yanayolenga kupunguza kasi ya kuenea kwa virusi, akipendekeza kufuta maagizo hayo mapema wiki ijayo.

Hadi kufikia sasa Marekani imeripoti maambukizi zaidi kwa Watu 55,148 ya virusi vya corona  ambavyo pia vimesababisha vifo vya watu 797.

Wakti hayo yakijiri Marekani, huko nchini India waziri Mkuu, Narendra Modi ameagiza wananchi wote (takribani Bilioni 1.3) kukaa nyumbani kwa muda wa siku 21 kuanzia leo, mkakati ambao unalenga kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona.

Senzo: Tutasajili kwa mapendekezo ya kocha
CORONA: Jiji la Kinshasa lafungwa, Rais atangaza hali ya dharura