Wananchi nchini Kenya wamefanya maandamano katika miji mikubwa nchini humo kutokana na kinachodaiwa kuwa ni kuchoshwa na vitendo vya maafisa wa serikali kuiba pesa zao na kuachiliwa huru.

Kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook na Twitter nchini humo kumekuwa na mijadala mbalimbali nchini humo inayolenga kupiga vita ufisadi na rushwa yenye mada ‘Hashtag’ zilizopewa majina ya; #TakeBackOurCountry, #STOPTheseTHIEVES, #SitasimamaMaovuYakitawala na #NotYetMadaraka.

Jumla ya watu 20 kati ya 50 waliokuwa wamekamatwa kutokana na sakata ya ufujaji wa Shilingi bilioni 8 ambazo ni mali ya Shirika la Vijana wa Huduma kwa Taifa (NYS) nchini Kenya wameshtakiwa lakini raia wanasema hawana imani kama wahusika watakabiliana na mkono wa sheria , kutokana na kwamba washukiwa katika sakata za ufisadi zilizofichuliwa vipindi vilivyopita waliachiliwa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Masuala ya Vijana na Jinsia Lilian Mbugua Omollo na Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Bw Richard Ndubai ni miongoni mwa walioshtakiwa huku pia mameneja wa kampuni ambazo zinadaiwa kuhusika katika ufujaji wa pesa hizo wakifikishwa kortini Milimani, Nairobi.

Katika siku za hivi karibuni serikali ya rais Uhuru Kenyatta imekumbwa na sakata la rushwa katika kile kianachoonekana kuwa ni kushindwa kwa juhudi za kupambana na ufisadi.

Zinedine Yazid Zidane ajiuzulu Real Madrid
Wazazi St. Florence waanza kuhamisha watoto wao

Comments

comments