Wananchi wa Kijiji cha kifumbe Kata ya Mahongole halmashauri ya Mji wa Makambako mkoani Njombe wameiomba serikali kutatua changamoto ya ubovu wa miundombinu ya barabara ambayo imepelekea kufungwa kwa soko la Nyanya lililopo kijiji jirani cha Usetule.

Wameyasema hayo wakati wakizungumza na Dar24 Media, ambapo wananchi hao wamesema kuwa kutokana na changamoto ya miundombinu ya barabara ambayo haipitiki imesababisha soko la Nyanya kufungwa kutokana na wafanyabiashara wa zao hilo kuishia mjini, hali ambayo imepelekea wananchi kushuka kiuchumi kutokana na nyanya zao kuozea shambani.

“Barabara kweli huku kwetu Kifumbe ni tatizo kutoka Makambako hadi huku kwetu pana takribani km 24 ambayo ni tatizo kubwa sana, kumekuwa na soko la nyanya lakini wameshindwa kuendesha biashara zao wakipeleka mazao pale sokoni tatizo kubwa barabara ni mbovu, mazao yetu yanabaki shambani kwa mfano wafanyabiashara wameshindwa kuja kununua mazao yetu mpaka nyanya zinaozea mtoni”wamesema baadhi ya wananchi

Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Anyetike Kasongo amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kuwataka wananchi wa kata hiyo kwa ujumla kuwa na subira kwa kuwa barabara hiyo itafanyiwa kazi ndani ya mwaka mpya wa fedha wa 2019-2020.

”Ni kweli barabara hiyo imekuwa na changamoto kwamba haijatengenezwa kwa miaka minne mfululizo lakini niwahakikishie wananchi kwa mwaka huu wa fedha tumeshaiingiza kwenye bajeti na itafanyiwa ukarabati mkubwa,kwa maana kwamba jumla ya km 48.9 kutoka Makambako mpaka Mtanga mpakani na halmashauri ya wilaya ya Mufindi kwa hiyo niwaombe tu wananchi kuwa na subira,”amesema Kasongo

Mwanamke Munira azinduka baada ya miaka 27 Hospital
Video: Kangi Lugola awataja wenye sifa za kusajili Laini za simu