Wananchi wanaoishi mipakani wametakiwa kutumia mipaka hiyo kufanya biashara na kujitajirisha kwa kufuata sheria, huku jukumu la serikali ni kuhakikisha wananchi wananufaika na si kuonekana kikwazo.
 
Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Prof. Faustine Kamuzora wakati akitembelea mipaka ya Tanzania na Uganda iliyopo Mkoani Kagera Wilayani Missenyi (Kabindi- Kashenye, Mtukula na Bugango) na Murongo Wilayani Kyerwa.
 
Amesema kuwa ni lazima Serikali kuyajua matatizo wanayokumbana nayo wafanyabiashara na kuyafanyia kazi ili wananchi wanufaike na fursa zilizopo katika mazingira yao, huku akiwataka watumishi wa Idara zote za Serikali zinazotoa huduma katika mpaka wa Mtukula kutokuwa kikwazo kwa wananchi wanaojishughulisha na biashara katika mpaka huo bali wawe wabunifu katika kazi zao.
 
Prof. Kamuzora amesema kuwa changamoto kubwa aliyoiona kwa upande wa pili wa nchi jirani ya Uganda wafanyabiashara wamekuwa wakichangamkia fursa karibu na mipaka kwa kuanzisha miji na vituo vya biashara wakati upande wa Tanzania kukiwa hakuna kilichoendelezwa na kupelekea Watanzania kunufaisha wenzao wa nchi jirani kwa kununua bidhaa huko.
 
“Sisi watumishi wa umma tusiwe kikwazo kwa watu wetu, kuwa mpakani ni fursa kubwa ya wananchi wetu kutajirika, ukienda nchi nyingine wananchi wa mipakani ndiyo matajiri kwasababu wamepewa fursa ya kufanya biashara katika pande zote mbili lakini kwa kuzingatia matakwa ya sheria,”amesema Prof. Kamuzora
 
Aidha, amesema kuwa kunatakiwa kufanyika upembuzi yakinifu na wa kina kuona kwanini nchi jirani wanatambua fursa za mipaka lakini sisi upande wa Tanzania bado hatutambui fursa hizo, huku akisisitiza kuwa kuna haja ya Serikali kuangalia upya mifumo ya kodi.
 
  • Neema Mgaya akerwa na mauaji Njombe,’Huu ukatili hauvumiliki’
 
  • Sakata la Korosho kaa la moto bungeni, ‘Mbunge aahidi kujiuzulu
 
  • Dkt. Bashiru amualika Lissu CCM
 
Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara wa mipakani waliokutana na Prof. Kamuzora wamemueleza kuwa upande wa nchi jirani ya Uganda, kodi zao ni nafuu katika kufungua biashara ukilinganisha na Tanzania na ndiyo maana maduka na biashara zianaanzishwa upande wa pili kuliko upande wa Tanzania.
 
Hata hivyo, Profesa Kamuzora amewashauri viongozi na Watendaji wa Halmashauri za Wilaya zilizopo mipakani kuona namna bora ya kuzibaini na kuzichambua chanagamoto mbalimbali zilizopo mipakani na kuishauri Serikali kwani wao ndiyo wanaishi katika maeneo husika kuliko viongozi waliopo Dodoma na Dar es Saam

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Februari 5, 2019
Video: Wakili Manyama amtaka Lissu ajitathimini,'Akigoma afutiwe ubunge'