Raia wa nchi ya Uganda na maeneo ya jirani wameingia hofu baada Serikali ya nchi hiyo kuthibitisha kuzuka kwa ugonjwa wa Ebola (EVD) na uwepo wa taarifa ya kifo cha mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 24, mkazi wa wilaya ya Mubende, iliyoko kilomita 150 magharibi mwa mji mkuu Kampala, ambaye aliaga dunia Septemba 19, 2022 kwa kuugua maradhi hayo.

Wananchi hao, wamesema hofu yao inatokana na tangazo la Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ya Uganda, Dkt. Diana Atwine aliyetoa maelezo kwamba mgonjwa aliyeporipoti hospitalini, alikuwa na dalili zinazoshukiwa kuwa ni za Ebola ambaye alitengwa ili kuchukuliwa vipimo Septemba 18, 2022 na matokeo yake yaliyotolewa jioni ya Septemba 19, 2022, yalithibitisha alikuwa na ugonjwa wa Ebola.

Uthibitisho huo, unafuatia uchunguzi wa timu ya watabibu wa Taifa wa kutafuta Majibu ya Haraka kuhusu vifo vinavyotiliwa shaka vilivyotokea Wilayani humo mwezi huu, ambapo Dkt. Atwine amesema, “Katika kijiji hicho hapo awali tumepata taarifa kuhusiana na vifo vya jamii, ambavyo wataalam wetu wa magonjwa walikwenda kubaini.”

Muhudumu wa Adfya akiwaongoza Wananchi waliofika kupata huduma. Picha na TRT World.

Ameongeza kuwa, “Kwa bahati nzuri, wengine hawakuthibitishwa, na aliyefariki alizikwa walakini, muundo wa tatizo hilo ulikuwa ndani ya familia moja yenye watu wazima watatu na watoto watatu.” huku shirika la Afya Ulimwenguni WHO likisema washukiwa wanane kwa sasa wanapokea huduma katika kituo cha afya.

Hata hivyo, Dkt. Diana Atwine amewataka wananchi kuwa watulivu, huku akiwasifia wataalamu wa Uganda kwamba, “Wuna uwezo, wana ujuzi, wanacho kila kinahitajika ili kudhibiti ugonjwa huo wa Ebola, kwa hiyo tunawaomba watulie na tuwajulisha kwamba tutashughulikia janga hili kwa usahihi.”

Ebola huenea kwa kugusana moja kwa moja na damu, viungo au majimaji mengine ya mwili ya watu walioambukizwa, kula nyama ya nyani au kutumia vitu kwa kuchangia na mgonjwa aliye na maambukizi huku Mamlaka nchini DR Congo iliyo jirani na Uganda ikisema Agosti, 2022 kisa kipya cha virusi hivyo kilihusishwa na mlipuko wa hapo awali.

Wafafanua Viongozi kutumia basi moja mazishi ya Malkia
Habari kuu kwenye magazeti ya leo Septemba 21, 2022