Wabunge wa Viti Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Njombe, Dkt. Suzan Kolimba pamoja na Neema Mgaya wamewasili katika kijiji cha Igwachanya na kutoa pole kwenye msiba wa kijana Ibrahimu Sanga aliyefariki dunia February 01 mwaka huu kwa kupigwa na wananchi wenye hasira huko katika Kata ya Usuka Wilayani Wanging’ombe akidhaniwa kuwa ni moja kati ya watekaji na wauaji wa watoto.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Igwachanya wilaya ya Wanging’ombe Mkoani Njombe. Adam Dononda amesema kuwa marehemu alikuwa mkazi wa kijiji na kata ya Igwachanya lakini tukio hilo limetokea katika kata ya Usuka maeneo ya Sekondari ambapo marehemu akiwa na rafiki yake walikutwa wamesimama na mwanafunzi wakike wa shule ya Sekondari ndipo wananchi wakapiga yowe na kukusanyika kufanya mauaji hayo.

Aidha, amemtaja kijana aliyekuwa na marehemu kuwa ni Given Nyachi ambaye amejeruhiwa vibaya kwasasa amelazwa katika Hospital ya Ikelu kwa ajili ya matibabu zaidi, huku mwili wa marehemu Ibrahimu umesafirishwa kwenda nyumbani kwao Jijini Mbeya kwa ajili ya mazishi.

Naye Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Igwachanya pamoja na wananchi wa kijiji hicho wamesema kuwa marehemu alikuwa fundi umeme kijijini hapo pia alikuwa akishirikiana vyema na jamii ya watu wa Igwachanya.

Kwa upande wake Dkt. Susan Kolimba na Neema Mgaya ambao ni wabunge wa viti maalum mkoa wa Njombe wameiasa jamii kuacha tabia za kujichukulia Sheria mikononi pindi wanapowahisi watu kuwa ni miongoni mwa vikundi vya wahalifu badala yake wawafikishe kwenye vyombo vya dola ili uchunguzi ufanyike.

Video: Mama anayedai kufika Mbinguni aomba msaada wa kidunia
Video: Wanawake Vinara mtandao wizi wa Bodaboda