Wafuasi wa kiongozi wa upinzani Senegal, Ousmane Sonko wamelaani ukatili uliokithiri unaofanywa na polisi baada ya majibizano kuhusiana na hukumu ya kifungo cha jela na kusababisha vifo vya watu 16 na zaidi ya waandamanaji 350 kujeruhiwa.

Ghasia hizo zilizuka wakati Sonko alipohukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani katika kesi ambayo anasema ililenga kumzuia kuwania urais nchini humo mwaka ujao huku wananchi wakisema wanahitaji msaada wa kisheria.

Shirika la Msalaba Mwekundu limesema limewasaidia waandamanaji 357 waliojeruhiwa akiwemo mwanamke mjamzito pamoja na askari 36 wa maafisa wa ulinzi na usalama waliojeruhiwa tangu ghasia zilipozuka.

Kwa ujumla watu 78 waliojeruhiwa vibaya walipelekwa katika vituo vya afya, iliongeza taarifa hiyo. Wafuasi wa Sonko na Rais Macky Sall wanatupiana lawama kwa ghasia na vifo hivyo.

Mayele afunguka atakapocheza msimu ujao
Rais Samia aipongeza Young Africans Ikulu