Kufuatia changamoto iliyokuwepo ya bei kubwa ya vifurushi vya mitandao ya simu, Mapema mwaka huu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile aliahidi maboresho kufikia Aprili 2, 2021, ambapo kanuni mpya za vifurushi vya simu zimeanza kufanya kazi leo Aprili 2, 2021.

Ikiwa leo ndiyo siku ambayo kanuni mpya zimeanza kufanya kazi hali imekuwa tofauti na matarajio ya wengi ambapo bei za vifurushi zimeonekana kupanda maradufu.

Baadhi ya watumiaji wa mitandao hiyo ya simu kupitia mitandao ya kijamii wameilalamikia mitandao ya simu kwa kufanya kinyume na matarajio ya wananchi wengi, hasa kutokana na maagizo ya Waziri mwenye dhamana.

Dar 24 Media inaendelea kuwatafuta wahusika wenye dhamana ya mawasiliano ili kupata ufafanuzi zaidi endelea kutufuatilia kupitia mitandao ya kijamii.

Ijumaa Kuu: Wakristo watakiwa kufuata sauti ya Mungu
Simba SC kuifuata mapema Al Ahly