Idadi ya watu walioripotiwa kujeruhiwa baada ya mlipuko wa bomu, uliotokea katika soko la Macampagne huko Beni mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imefikia 37 huku Wananchi wakiiomba Serikali ya nchi hiyo kutafuta suluhu ya amani.

Mkuu wa Wilaya ya blue-collar, amesema kuwa majeruhi katika tukio hilo walipelekwa kwenye vituo vya vya afya kwaajili ya kupatiwa matibabu na kwamba wengi wao walikuwa ni wafanya biashara.

Moja ya ajali zilizotokea wakati wa shambulizi hilo. Picha ya Africanews.

Beni, ni mojawapo ya maeneo yenye hali tete mashariki mwa DRC, ambayo yamekuwa yakikumbwa na ukosefu wa usalama kwa takriban miaka 30 sasa.

Januari 15, 2023 shambulio la Allied Democratic Forces (ADF), kundi lenye mfungamano na wanajihadi wa kundi la Islamic State, liliua takriban watu 15 katika kanisa la kiinjili la Kiprotestanti la Kasindi.

Simba SC: Tunamsaka Mkurugenzi wa Ufundi
Kiongozi wa ISIS auawa na Wanajeshi wa Marekani Somalia