Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa mwelekeo wa hali ya hewa kwa kipindi cha Juni hadi Agosti mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini dar es salaam meneja kituo kikuu cha utabiri Samwel Mbuya amesema Nchi inatarajia kuwa na hali ya baridi kiasi katika kipindi hiki sambamba na vipindi vifupi vya mvua vinavyotarajiwa kujitokeza katika maeneo machache hususani ukanda wa Ziwa Viktoria na ukanda wa pwani ya Kaskazini.

Inatarajiwa Katika kipindi cha mwezi Juni hadi Agosti 2016, maeneo mengi ya nchi yanarajiwa kuwa makavu na yenye hali ya baridi kiasi katika majira haya yakipupwe.

Mifumo ya hali ya hewa inaonesha matarajio ya hali ya joto la wastani hadi chini ya wastani katika maeneo yaliyopo Kusini-magharibi mwa nchi.

Aidha amesema sababu za hali hiyo ni pamoja na kupungua kwa joto la bahari katika eneo la ukanda wa Tropiki la bahari ya Pasifiki sambamba na Joto la baharí.

katika eneo la magharibi wa bahari ya Hindi kuwa la wastani kwa kipindi cha miezi ya Juni hadi Agosti 2016

kwa upande mwengine, Afisa Uhusiano wa TMA, Monica Mutoni ametoa msisitizo kwa wananchi kufuatilia taarifa zinazotolewa na Mamlaka kupitia vyombo mbalimbali vya habari, tovuti ya Mamlaka ili kuokoa maisha na mali.

Mara kwa mara Kumekuwa na mabadiliko ya hali ya hewa nchini hivyo ni vema wananchi kuchukua tahadhari kwa mabadiliko yanayoweza kujitokeza.

Majaliwa: Mpango wa pili wa maendeleo unalenga kuboresha maisha ya maskini
Rais Magufuli amteua Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu