Wananchi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wametakiwa kuacha tabia ya kukaa kimya kwenye masuala mbalimbali yahnayohusu mianya ya rushwa kwa kuhofia uhai wao na badala yake wanatakiwa kutoa taarifa kwa vyombo husika.

Kwa sasa pamoja na kwamba baadhi ya nchi wanapambana na rushwa bado kuna maeneo wanaendelea kutoa na kupokea rushwa.

Hayo yameelezwa hivi karibuni na Mwenyekiti wa Kamati ya usuluhishi na migogoro kutoka katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA). Victor Burikukiye wakati akiongea na wajumbe wa kamati hiyo.

Amesema kuwa hali hiyo ya rushwa kwa baadhi ya maeneo imesababisha wananchi au walengwa kushindwa kupatiwa haki zao za msingi.

Aidha, amesema kuwa ipo haja sasa kwa walengwa ambao ni wananchi kuacha uoga na badala yake kutoa taarifa kwa vyombo vinavyousika ili kuepusha majanga ambayo yanaweza kutokea.

“Ni ngumu vyombo vya dola kuweza kubaini mambo yote kwa wakati mmoja ila kama watapewa ushirikiano wanaweza kutatua matatizo hayo ya uombaji au utoaji wa rushwa,”amesema Burikukye

Hata hivyo, ameongeza kuwa hata nchi wanachama nazo zinatakiwa kuongeza wigo mpana ikiwa ni pamoja na kuwa na mbinu ambazo zitakuwa raisi kutolea elimu ya masuala ya rushwa.

Jiji la Dar kuwa mwenyeji wa mashindano ya AFCON
Video: Dkt. Bashiru 'Serikali ya 2010 ilikosa uhalali kisiasa', Watoto 61 wapotea ndani ya siku 90