Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Salama Mbarouk Khatib ametoa onyo kwa watu wanaochukua mchanga wa kaburi la Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad kwani utaratibu huo haukubaliki

Marufuku hiyo ya Khatib inafuatia tabia ya watu wanaokwenda kumuombea Dua Maalim Seif aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, kuchukua mchanga wa kaburi kwa madai unanukia Miski.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, RPC Juma Sadi Khamis amesema watu wanaruhusiwa kwenda kumuombea dua marehemu lakini amewaonya kuchukua mchanga wa kaburi kwa sababu yoyote.

Maalim Seif Sharif Hamad ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, alifariki dunia Februari 17, 2021.

Kenya kinara utakatishaji Fedha Afrika Mashariki
Mrema: Mimi ni mzima wa afya